. . . Kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, hayatamfikia yeye. —ZABURI 32:6
Ni rahisi: Kadri unavyotumia muda mwingi na Mungu, ndivyo unavyojiunganisha kwa nguvu zake. Daudi anatuambia kwamba, ni katika mahali pa siri pa uwepo wa Mungu ambapo tunalindwa (Zaburi 91:1). Tunapotumia muda katika uwepo wa Mungu, katika maombi, na katika Neno lake, tuko katika mahali pa siri. Mahali pa siri ni mahali pazuri pa amani na utulivu!
Inatia nguvu kujua kwamba wema wa uwepo wa Mungu upo kwa ajili yetu waaminio. Hili likiwa akilini, ni kitu gani ulimwenguni kitakachotuzuia kutumia wakati wetu na Mungu? Hata Yesu alikuwa akiamka asubuhi mapema kuwa peke yake na Mungu. Tunakuwa na nguvu na hekima tu kwa kuwa na Mungu!
Kitu kizuri cha kufanya ni kutoa kiasi fulani cha muda wako ili kuwa na Mungu. Usilifanye kuwa kama sheria, lakini jaribu kulifanya mara kwa mara kadri unavyoweza. Zungumza na Mungu kuhusu kitu chochote na vitu vyote vilivyo moyoni mwako— anajali maslahi yako yote yanayokujalisha au wasiwasi yako. Huenda wakati mwingine unataka kusikiliza muziki na sifa; na huenda nyakati zingine ukataka tu kukaa kwa utulivu na kufurahia kimya. Tenga wakati wa kuwa na Mungu na uruhusu Roho Mtakatifu kukuongoza katika safari ya kushangaza ya kumkaribia Mungu!
Kutumia muda katika mahali pa siri pa uwepo wake hukubadilisha kutoka ulicho hadi kile mwenyewe anaweza kukuumba kuwa.