Wakati wa Kukumbuka

Wakati wa Kukumbuka

Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, na Mungu aliye juu ni mkombozi wao. ZABURI 78:35

Kuna nyakati za kusahau na vitu vya kusahau. Kwa mfano, Mtume Paulo aliposema kwamba aliyasahau yaliyo nyuma, alikuwa akiongea kuhusu kutohisi kuhukumika kwa ajili ya makosa ya nyuma (tazama Wafilipi 3:13). Katika Isaya, tunafundishwa tusikumbuke vitu vya kale kwa sababu Mungu anafanya kitu kipya. Hiyo ina maana tu tusikwame katika mambo ya nyuma.

Tunasikia mafundisho mengi kuhusu kusahau ya nyuma, na ingawa kuna nyakati za kufanya hayo, tunafaa pia kufundishwa kukumbuka kwa shukrani mambo yote mema ambayo Mungu ametufanyia, na kupitisha shukrani hzio kwa vizazi vijavyo. Moyo wenye shukrani ni moyo ambao hukumbuka upendo wa Mungu na matendo ya ajabu na kuupa ulimwengu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa vitu vya ajabu ambavyo ulinifanyia. Nisaidie kukukumbuka wema wako wakati wote na kuutumia kujenga imani yangu kwa ajili ya vitu vikubwa vizuri zaidi vinavyokuja.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon