Wakubali Watoto Wako Jinsi Walivyo

Wakubali Watoto Wako Jinsi Walivyo

Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. WAEFESO 6:4

Upendo na kukubaliwa ndivyo vipaji vikubwa sana ambavyo wazazi wanaweza kuwapa watoto wao. Kukubaliwa huwaweka watoto wetu huru na kuwaruhusu kuwa kile Mungu aliwaumba kuwa. Upendo huona vipaji vilivyo ndani ya watoto wetu, shukuru Mungu kwa vipaji hivyo, na kutafuta kuwasaidia kutumia vipaji hivyo kwa utukufu wa Mungu.

Ili kuwa na uhusiano chanya wa amani na watoto wetu, ni muhimu kabisa kwamba—hata kama tunawakosoa—tuwakubali jinsi walivyo na kwamba tukumbatie nafsi zao za kipekee. Upendo haujaribu kuwalazimisha watoto wetu kuwa kile tunachotaka wawe. Huwasaidia kuwa kile Mungu anataka wawe, na kushinda udhaifu wao na kunawiri katika kutumia nguvu zao.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwa watoto ulionipa na vipaji na nafsi za kipekee alizo nazo kila mmoja. Nipe hekima ya kuwalea vizuri niwezavyo kwa utukufu wako. Ninashukuru sana kwamba umewaweka katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon