Watatu Ndani ya Mmoja

Naye Roho ndiye ashudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli, kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni, Baba na Neno na Roho Mtakatifu , na watu hawa ni umoja. (1 YOHANA 5:7-8)

Andiko linazungumza kuhusu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu- ambao tunajua kama Utatu Mtakatifu. Ingawa andiko halitumii neno Mwana, linamrejelea Yesu kama “Neno,” lakini tunajua kutokana na Yohana 1 kwamba Yesu na Neno ni mmoja na yule yule.

Tunapofikiria kuhusu utatu, lazima tukumbuke kwamba ni watatu na ilhali ni Mmoja. Hili haliingiani kihesabu, lakini ni ukweli kulingana na maandiko. Kwa kuwa na Roho Mtakatifu akiishi ndani yetu, pia nasi tuna Baba na Mwana wanaishi ndani yetu.

Huu ni ukweli halisi. Ni jambo la ajabu sana kueleza. Lazima tu tuliamini kwa mioyo yetu. Usijaribu kulielewa. Kuwa kama mtoto mdogo na uliamini tu kwa sababu Biblia inasema hivyo: Utatu wote- Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu- unaishi ndani yako na mimi na kila aaminiye ambaye amemkubali Yesu kama Mwokozi na Bwana wake (soma Wakolosai 2:9-10).

Ukweli huu unafaa kutufanya tuwe wajasiri, bila woga na wajasiri kwa njia ya kiasi. Tunafaa kuamini tunaweza kufanya tunachohitaji kufanya katika mpango wa Mungu juu ya maisha yetu kwa sababu Utatu Mtakatifu hutuandaa. Hutupatia kila kitu tunachohitaji na vingi zaidi. Mungu anakupenda, yuko nawe kila wakati, na ana mpango mzuri juu ya maisha yako. Kupitia kwa uwepo wake, umeandaliwa kufanya unachohitaji kufanya katika maisha.  

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kabili hii siku kwa ujasiri kwa sababu tayari Mungu amekuwa unakoenda na ameandaa njia.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon