Weka Siri za Mungu

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini, na Baba yako aliye sirini atakujazi (MATHAYO 6:6)

Nimekuja kugundua katika kipindi cha muda mrefu cha tajriba yangu na Mungu kwamba hatuna usiri wa mambo yanayofaa kuwa siri. Andiko la leo linaonyesha kwamba, tunachoomba kuhusu kiko kati yetu na Mungu na hakihitajiwi kufanywa kama onyesho kwa wengine. Tunataka kusikia kutoka kwa Mungu ilhali wakati tunaohisi kuwa ametuambia chochote, tunaanza kuwaambia wengine alichosema. Pengine hilo ni sawa wakati mwingine, lakini kuna nyakati ambazo vitu kati yetu na Mungu vinahitaji kuwekwa kama siri.

Yusufu alipokuwa na ndoto kuwa babake na ndugu zake watamwinamia siku moja, pengine ulikuwa upumbavu wa kitoto uliomchochea kuwaambia kuhusu ndoto hiyo. Pengine ulikuwa huo ujinga ambao Mungu alitaka kuondoa ndani ya Yusufu kabla ya kumwamini na wajibu aliokuwa nao akilini mwake. Mara nyingi kutoweza kwetu kuweka siri ni ishara ya kutokukomaa. Ninafikiri tunaweza kuona tuzo za Mungu zikidhihirika katika maisha yetu, jinsi andiko la leo linavyosema, iwapo tutajifunza kufanya utambuzi kati ya kile tunachoweza kusema na kile cha kuweka kama siri.

Mungu atafunua mengi kwetu iwapo anaweza kutuamini. Acha tujifunze kushikilia mambo mioyoni mwetu hadi Mungu atupe ruhusa ya kuyaachilia.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa mwangalifu wa kile unachosema hisia zako zinapochochewa.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon