Yesu Alituonyesha Njia

Yesu Alituonyesha Njia

Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. WAEBRANIA 13:8

Katika sehemu yoyote ya maisha, Yesu ndiye mfano wetu—na Yesu wakati wote alionyesha uthabiti wa kihisia. Biblia inamrejelea kama “Mwamba,” na tunaweza kumtegemea ili tuwe imara, thabiti, na madhubuti—sawa—wakati wote. Huwa mwaminifu, mwajibikaji na mkomavu wakati wote na mkweli kwa Neno lake.

Yesu hawi katika hali moja ya kihisia leo na katika hali nyingine ya kihisia siku inayofuatia. Shukuru kwamba tunaweza kumtegemea kuwa yuleyule leo vile alivyokuwa jana na kuwa yuleyule kesho jinsi alivyo leo. Kuweza kutegemea uthabiti wa Yesu na kutobadilika ni miongoni mwa sifa zinazofanya uhusiano naye uonekane wa kuvutia kwetu. Iwapo tutajifunza kuwa wenye shukrani kwa mfano ambao Yesu alituonyesha, na kufuata mwongozo wake, tutaweza kujifunza kuwa imara na kufurahia maisha zaidi.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba sihitaji kutawaliwa na hisia. Asante kwa mfano wa Yesu. Nisaidie kuwa thabiti na madhubuti bila kujali kinachoendelea mahali nilipo. Nisaidie kuwa kama Yesu zaidi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon