Yesu, Mfalme wa Amani

Yesu, Mfalme wa Amani

Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. —YOHANA 14:27

Tunapofadhaika, huwa tunajaribu kuondoa vitu vinavyosababisha matatizo yetu. Lakini chanzo cha mfadhaiko si haswa matatizo, hali na mazingira. Mfadhaiko huja tunapokabiliana na matatizo kwa mtazamo wa ulimwengu badala ya kuwa na imani ndani ya Yesu Kristo, Mfalme wa Amani.

Ni damu ya Yesu iliyonunua amani yetu. Amani ni yetu kama zawadi kutoka kwake, lakini tunahitaji kuwa na azma ya kubadilisha mtazamo wetu wa maisha. Hatuwezi kuwa na mfadhaiko, masikitiko, uchungu, ugomvi na kukwazika, au tusiobadilika, wenye fikra za kisheria na tufurahie amani ya Mungu.

Hata kama bado tutakuwa na masuala yanayokera kukabiliana nayo, tunaweza kuwa na amani ya Yesu kwa sababu ameshinda ulimwengu na kunyima ulimwengu nguvu zake za kutudhuru (Yohana 16:33). Alituacha na nguvu za “kukoma kujiruhusu” kuwa na wasiwasi na kukereka!” Amani ipo; unachohitaji kufanya ni ichague!

Mfalme wa Amani, Yesu, ambaye anaishi ndani ya wale waliompokea, anajua na atatufunulia hatua muhimu tutakazochukua katika kila hali ili atuongoze katika amani.

Ni ajabu ilioje, mambo tunayoweza kukamilisha ndani ya Yesu iwapo tutaishi siku moja kwa wakati mmoja katika amani yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon