Una Tumaini na Siku za usoni

Una Tumaini na Siku za usoni

Yeremia 29:11, maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Je, si ni jambo la kufurahisha kujua kwamba kuna mpango wa maisha yako? Hajalishi yale yametendeka maishani mwako, hatua zile ulienenda vibaya, la muhimu ni kujua kwamba Mungu amekuongoza hadi hapa sasa. Amekuwa akikuongoza kwake mwenyewe. Ukweli ni kwamba tumaini lako kamili na hatima yako iko ndani yake.

Hii inamaanisha kwamba unaweza kuyaishi maisha yako yote kwa ajili ya Yesu na ndani yake. Na kw ajili yake, na ahadi yake kwamba hatakuacha, sasa kuna jambo la kusisimua.

Ni safari, safari ya umilele

Unaweza kuwa unauliza, je sasa nitafanya nini kwa vile nimempokea Kristo? Ni swali muhimu mno kwa vile umechukua hatua ya kwanza. Hata ingawa leo hautajihisi tofauti, jua kwamba Kristo ameanza kutenda kazi ndani yako.

Wakolosai 2:6-7 inasema, Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;  wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.

Shina hiyo hujengeka kupitia maombi, kusoma neon la Mungu, Bibilia and kumruhusu Roho Mtakatifu akuongoze na kukuelekeza.

Kuanza maisha yako na Kristo

Ahadi ya neon la Mungu, haya ndiyo maneno ya Yesu kwa wanafunzi: Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

Umeitwa kuishi maisha ya ukamilifu nay a kufurahisha katika Kristo nasi tuko hapa kukusaidia kuanza safri yako kwa nguvu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon