Kibali cha Kimiujiza

Kwa maana wewe utambariki mwenye haki; Bwana utamzungushia radhi kama ngao. —Zaburi 5:12

Nilipoanza kuhubiri kwa mara ya kwanza, niliogopa. Nilihofia kukataliwa. Katika siku hizo, kwa mwanamke kuhubiri lilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo sasa ambapo wahubiri wanawake sasa wanakubalika kote. Kwa hivyo nikahubiri vile nilifikiri nilitarajiwa kuhubiri.

Tatizo lilikuwa kwamba, nilikuwa nikijaribu kupata kibali cha watu kupitia kwa bidii yangu lakini sikufaulu. Kujaribu kupata kibali wewe mwenyewe sio tu kazi ngazi ngumu, mara nyingi huwa haina maana. Kadri unavyojaribu, ndivyo watu wachache wanavyovutiwa upande wako.

Wakati huo, sikujua lolote kuhusu kibali cha kimijiuza. Sikujua kuwa kibali ni sehemu mojawapo ya neema. Kwa kweli, katika Agano jipya la Kiingereza, maneno neema na kibali yote yanatasiriwa kutokana na neno la kiGiriki charis. Kwa hivyo neema ya Mungu ni kibali cha Mungu. Na neema ya Mungu husababisha vitu vinavyohitaji kufanyika katika maisha yetu kufanyika. Neema ni nguvu za Mungu zijazo kupitia kwa imani yetu kufanya tusioweza kufanya peke yetu. Sio kwa uwezo wa binadamu au nguvu za binadamu, bali kwa Roho Mtakatifu ambapo tunapokea. Ni kwa Roho wa Mungu wa neema ambapo huwa tunapata kibali na Mungu na mwanadamu.


Tangaza kwa sauti kila siku kwamba unaamini una kibali na Mungu na kwamba anakupa kibali na mwanadamu! (Mithali 3:4)

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon