Jinsi ya Kumjua Yesu How to Know Jesus

Jinsi ya Kumjua Yesu

Unapomjua Yesu, utaanza safari yako katika kuelewa mpango wa Mungu juu ya maisha yako. Romans 3:23 inayasema haya hivi: Kwa maana wote wametenda dhambi na kupungikiwa na utukufu wa Mungu.

Kumjua Yesu ni kutambua haja yako ya kuwa naye, kuamini yale anayosema na kuipokea zawadi hii ya ajabu. Inatambua kwamba huwezi kuyamudu maisha haya pekee yako, na kwamba umetenda dhambi na una hitaji ya Mwokozi.

Na habari njema kuhusu kumjua Yesu, na kuokoka ni ile hali ya kubadilishwa kunakotendeka mara hiyo. Unampa mambo yote mabaya na dhambi ulizotenda, naye Mungu anakupa yote aliyo nayo. Uwe unajua au usijue, Mungu ana mpango mzuri juu ya maisha yako, na hii ni hatua ya kwanza muhimu sana.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.  —Yohana 3:16

MAOMBI

Warumi 10:9 inasema kwamba ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

 

Ikiwa Yesu anakuita kuwa na uhusiano wa karibu naye, na uko tayari kumfuata katika yote utendayo, omba hivi kwa sauti:

 

“Yesu, ninajua nimetenda dhambi na ninamhitaji Mwokozi. Ninaamini kwamba ulipoenda msalabani, ulienda kwa niaba yangu, na dhambi zangu zote. Ninakuamini kwamba unaweza kuniokoa. Ninakupa maisha yangu. Leo,ninaamini nimeokoka, nisaidie kuelewa maana ya kukuishia kila siku. Amina.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon