TUMAINI kwa nyakati ngumu

TUMAINI kwa nyakati ngumu

Unapita katika kipindi kigumu? Iwe unashughulikia msiba au tatizo ambalo haukulitarajia, ugonjwa wa kutisha unaohitaji matibabu, au hata unajiuliza mlo wako unaofuata utatoka wapi, Mungu hataki ukabiliane na vita ukiwa peke yako. Badala yake, jambo kuu moja tunaloweza kufanya ni kumwamini Yeye, tukijua kuwa yuko pamoja nasi na tunaweza tukabaki tukiwa tumejaa matumaini.

Katika kitabu hiki, Joyce anafundisha:

  • Namna ya kupokea faraja ya Mungu katika nyakati ngumu
  • Kwa nini mabadiliko ya mtazamo yanaweza yakaibadilisha kabisa siku yako
  • Namna ya kuanza upya na kusahau mambo ya zamani
  • Funguo za Kibiblia za kupambana na unyogovu na kuvunjika moyo

Chochote ulichopitia, kitabu hiki kitakusaidia kuongeza matarajio yako na usikate tamaa kwa Mungu kamwe. Kwa sababu, zaidi ya yote, Yeye ndiye “Mungu wa tumaini” (Warumi 15:13), na Yeye ndiye anaweza kuichukua hali yako na kuibadilisha kuwa kitu kizuri zaidi.

Tumaini Dhabiti

Mungu hufurahia kutushangaza na atafanya hivyo kila mara iwapo tutaachilia vitu katika mikono yake na usalama wake. Anataka tushirikiane katika maisha yetu, na tukimruhusu kufanya hivyo, nafsi zetu zinaweza kuwa na utulivu.
MAGEUZI YA UPENDO

MAGEUZI YA UPENDO

Ninapokaa na kunywa kahawa yangu asubuhi, nikiangalia kupitia...
Nisaidie-Ninaogopa!

Nisaidie-Ninaogopa! (629KB)

Ujumbe huo, “Usiogope, kwa maana Mimi Mungu, niko pamoja nawe,” umeashiriwa mara nyingi sana katika Biblia.
Nisaidie-Nina Upweke!

Nisaidie-Nina Upweke! (798KB)

Mungu angependa ufahamu kuwa wewe huko peke yako. Shetani naye angependa uamini kwamba uko peke yako, lakini hii si kweli.
Lini Mungu Lini

Lini Mungu Lini (840KB)

Katika sura hii, mwandishi wa Zaburi ansema kwamba alimtumainia Mungu kumkomboa, na alimtegemea kufanya hivyo kwa wakati uliofaa.
WAAMBIA NINAWAPENDA

WAAMBIE NINAWAPENDA (730KB)

Mungu anataka kuwa na jamii, na anataka kuwa Baba yetu.
UAMUZI MUHIMU ZAIDI UTAWAHI KUHANYA

UAMUZI MUHIMU ZAIDI UTAWAHI KUFANYA (1MB)

Ningependa kuzungumza nawe kuhusu uamuzi muhimu zaidi...
KUWA NA MATUMAINI

KUWA NA MATUMAINI (1MB)

Mara kwa mara watu huhisi kuwa mtu akitarajia zaidi ya alivyo navyo basi ni mlafi au anafanya makosa...
KWA NINI, MUNGU, KWA NINI?

KWA NINI, MUNGU, KWA NINI? (1MB)

Je, umechanganyikiwa? Kuna kitu kinachotendeka maishani mwako sasa hivi ambacho hukielewi...
Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon