Kumfuata Mungu Hatua Moja kwa Wakati Mmoja

Kumfuata Mungu Hatua Moja kwa Wakati Mmoja

Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, naye aipenda njia yake. ZABURI 37:23

Ukitaka Mungu akutumie, usiruhusu hofu ya kushindwa kukuzuia kumtii anapokuongoza. Shukuru kwamba Mungu haoni tu ulipo, huona mahali unaweza kuwa. Haoni tu ulichotimiza, anaona utakachofanya na usaidizi wake. Wakati wote Mungu hutuongoza kwenye mambo makubwa na hutaka tutazamie mbele kwa siku zijazo. Usiogope usiyoyajua kwa kuwa Mungu anajua kila kitu, na uko salama naye.

Mara nyingi kumfuata Mungu ni kama kutembea kwenye ukungu. Tunaweza kuona tu hatua moja au mbili mbele yetu, lakini tunapochukua hatua hizo, inayofuatia inakuwa dhahiri. Tunapomwamini Bwana, tutakuwa na safari ya kusisimua itakayofanya maisha yawe yenye vituko na kufurahisha—katika kila hatua njiani.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kuwa unaelekeza na kuimarisha hatua zangu. Ninakuamini kuniongoza hatua mmoja kwa wakati mmoja hadi kwenye kusudi ulilo nalo juu yangu. Asante kwa kuwa una vitu vizuri ulivyopanga kwa ajili ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon