Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri. —Zaburi 51:6
Mungu anataka tukabiliane na ukweli katika utu wetu wa ndani, halafu pengine tuukiri kwa namna inavyofaa kwa mtu anayestahili. Na wakati mwingine ni sisi tunaohitaji zaidi kusikia ukweli.
Watu wanapokuja kwangu ili niwape usaidizi katika eneo hili, mara nyingi huwa nawaambia “Nenda ukajitazame kwenye kioo na ujieleze tatizo mwenyewe.” Kuwa mwaminifu kwako binafsi hukuweka huru!
Iwapo kwa mfano, tatizo lako ni kwamba wazazi wako hawakukupenda ukiwa mtoto na ukachukizwa na kuwa na uchungu, kabiliana na ukweli uliopo mara moja kabisa. Jitazame kwenye kioo na useme, “Wazazi wangu hawakunipenda, na pengine hawatawahi kunipenda. Lakini Mungu ananipenda, na hilo linatosha!”
Usiwe ukaja kuwa mmojawapo wa watu wanaoishi maisha wakijaribu kupata kitu ambacho hawatawahi kupata. Iwapo umeruhusu ukweli kuwa hukupendwa uharibu maisha yako kufikia hapa, usiachilie uharibu maisha yako yaliyobaki. Unaweza kufanya vile Daudi alifanya. Jieleze: “Ingawa baba na mama yangu waliniacha, bali Bwana atanikaribisha kwake [atanichukua kama mwanawe]” Zaburi 27:10. Kabiliana na tatizo lolote linalokusumbua, fikiria kumwambia msiri unayemwamini, halafu ujieleze mwenyewe binafsi katika utu wako wa ndani.
Kukubali ukweli hufanya yaliyopita kupoteza nguvu juu yetu.