Karama ya Kuponya

…na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja.. (Wakorintho 12:9)

Karama ya kuponya hufanya kazi pamoja na karama ya imani. Hata ingawa waaminio wote wanahimizwa kuombea wagonjwa na kuona wakipata nafuu (soma Marko 16: 17-18), Roho Mtakatifu hugawa karama za kuponya zisizo za kawaida kwa baadhi ya watu, jinsi anavyowapa watu fulani karama zingine za kiroho.

Katika makongamano yetu, huwa tunawaombea watu na kuona uponyaji wa ajabu. Kwa muda wa miaka mingi, tumepokea ushuhuda chungu nzima na ripoti za uponyaji wa mwili uliothibitishwa. Huwa ninaomba maombi ya imani wakati wa makongamano yetu na katika vipindi vyetu vya runinga na nina imani kwamba Mungu hutenda.

Mtu anapopokea uponyaji kupitia kwa karama ya kiroho, huenda uponyaji huo usionekane mara moja. Uponyaji unaweza kuwa mchakato ambao hufanya kazi kama dawa. Ni muhimu kuupokea kwa imani na kuamini kwamba unafanya kazi. Matokeo mara nyingi huonekana baadaye. Huwa ninahimiza watu kusema, “Nguvu za uponyaji wa Mungu zinafanya kazi ndani yangu sasa hivi.”

Tunafaa kuamini Mungu katika eneo la afya yetu. Ninamshukuru Mungu kwa sababu ya madaktari na dawa ninapozihitaji, lakini Yesu ndiye Mponyaji wetu (soma Isaya 53:5).

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu ndiye daktari wako na Neno lake ni dawa yako. Mwambie akuponye kwa kila njia.   

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon