Kujifunza Kutarajia Wema wa Mungu

Kujifunza Kutarajia Wema wa Mungu

Kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga… YAKOBO 1:17

Mungu hufurahia kuwakimu wanawe. Lazima tutambue kwamba anapenda kutubariki na tujifunze kuishi tukishukuru kwa wema wake. Hii hapa orodha ya vitu vya kufikiri na kuongea kuhusu upaji wa katika maisha yako:

  • Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu (tazama Wafilipi 4:19).
  • Mungu hunibariki ili niwe baraka kwa wengine (tazama Mwanzo 12:2).
  • Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika (tazama Luka 6:38).
  • Mungu hutupa vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha (tazama 1 Timotheo 6:17).
  • Ninamtumikia Mungu naye hupendezwa na mafanikio yangu (tazama Zaburi 35:27).

Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa upaji wako mwingi katika maisha yangu. Ninashukuru kwamba unakimu kila hitaji langu. Nisaidie kuamini wema wako katika maisha yangu na kujifunza kukutazama wewe kwanza kutimiza kila hitaji langu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon