Kupanda Mbegu za Ushindi

Kupanda Mbegu za Ushindi

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu. Waefeso 3:20 Biblia

Mojawapo ya hofu kuu na isiokoma ambayo watu wengi huwa nayo ni woga kwamba hawatakuwa na kile wanachohitaji cha kutosha. Tunataka kuhisi usalama katika kila eneo la maisha. Tunataka kuwa salama katika imani yetu kwamba tutakuwa na kile tunachohitaji tunapokihitaji. Hofu inaweza kusababisha moyo usio na shukrani, kwa sababu inaleta hisia kwamba hakuna vya kutosha. Ni vizuri kuuliza Mungu tunachotaka na kuhitaji halafu tufikirie kuhusu tulicho nacho badala ya kile tusicho nacho.

Neno la Mungu linasema kwamba tusihofu kwa kuwa yuko nasi. Ni rahisi tu hivyo: “Usihofu” (Hakuna cha kuhofu), kwa kuwa ni pamoja nawe” (Isaya 41:10). Shukuru kwamba ana kila kitu tunachohitaji na anatupenda. Kwa hivyo kama mzazi yeyote anayewapenda wanawe, atatimiza haja zetu. Ameahidi kuwa hatatuacha wala kutupungukia. Tunaweza kushukuru kwamba huwa halali, yuko nasi daima, na hutuangazia macho yake kwa upendo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unanipa vyote ninavyohitaji na mengine mengi. Ninakataa kuishi katika hofu, huku nikishangaa iwapo nitawahi kuwa na vya kutosha. Asante kwa kuwa wewe ni Mungu afanyaye ya ajabu mno kuliko yote ninayoweza kuomba au kuwaza.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon