Kuweka Imani Yako Mahali Panapofaa

Kuweka Imani Yako Mahali Panapofaa

Hawa wanataja magari na hawa farasi, bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu. —ZABURI 20:7

Kuna sura nyingi za imani. Hata hivyo iliyo nzuri sana ni tumaini! Tumaini ni kitu tulicho nacho, na huwa tunaamua tunachotaka kufanya nalo. Huwa tunaamua tutakayeweka tumaini letu ndani yake ama ni kitu gani tutakachoweka tumaini letu.

Umeweka tumaini lako wapi? Tumaini lako liko ndani ya kazi yako, mwajiri, akaunti ya benki, au marafiki? Pengine tumaini lako liko ndani yako binafsi, rekodi zako za ushindi, elimu, vipawa vya kiasili, ama mali. Hivi vyote ni vya muda tu, na vinavyoweza kubadilika. Ni Bwana tu asiyebadilika. Ni yeye peke yake ndiye Mwamba usiyoweza kutingizwa.

Kama watoto wa Mungu, tunaweza kuwa na hakikisho kuwa Mungu atatuokoa kutokana na mashaka yaliyopo, vile tu alivyotuokoa katika siku zilizopita. Hivyo basi tunaweza kuchukua tumaini letu na kuliweka mahali panapofaa, ambapo ni ndani ya Mungu peke yake.

Tumaini halifadhaiki kwa kuwa limeingia katika raha ya Mungu.

Tumaini halijachanganyikiwa, kwa sababu halina haja ya kutegemea akili zake lenyewe. Tumaini halikati tamaa wala kushikwa na woga. Tumaini huamini kwamba Mungu ni mwema na kwamba hutenda mambo yote ili kutupatia mema!


Chagua kuweka tumaini lako ndani ya Mungu. Hulipa faidi ya ajabu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon