maisha ya nidhamu italeta amani ya Mungu

maisha ya nidhamu italeta amani ya Mungu

Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Waebrania 12:11

 Mambo mengi yashindana kwa rasilimali zetu ndogo za muda, nishati na wakati. Nilikuwa ninalalamika kwa Mungu juu ya ratiba yangu kuwa kubwa. Ningelia sana, “Mungu, ni nani anayeweza kunitarajia kufanya yote ninayoyafanya?”

Kisha ikanijia: Mimi ndio nilifanya ratiba yangu na hakuna mtu anayeweza kuibadilisha isipokuwa mimi! Sikuweza tena kutumia wakati kutaka mambo yawe tofauti kwa sababu hiyo haingebadilisha chochote.

Mungu alinionyeshea kuwa nilipaswa kujipa nidhamu mwenyewe ili kurahisisha maisha yangu.

Utahitaji kufanya hivyo pia ikiwa unataka kupunguza mwendo wa maisha. Umuulize Roho Mtakatifu akusaidie. Anaweza kukuongoza, akikuonyesha mambo ya kufanya na ni yapi ya kuacha.

Inaweza kuwa ngumu mara ya kwanza, hasa ikiwa hujajipa nidhamu katika siku za nyuma, lakini malipo ya nidhamu na kujizuia yanafaa jitihada yako.

Biblia inasema kwamba nidhamu huleta matunda ya amani. Anza kujipa nidhamu leo, na unaweza kuanza kufurahia maisha ya amani ambayo Mungu amekuandalia.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nataka kupata matunda ya amani ya maisha mazuri. Wakati ninapojaribiwa kujiinua na kujinyoosha mbali sana, nisaidie kupunguza mwendo na kufanya tu mambo unayotaka nifanye.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon