Mungu Anakupenda na Huona Wema Ulio Ndani Yako

Mungu Anakupenda na Huona Wema Ulio Ndani Yako

Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehasabiwa zote. MATHAYO 10:29–31

Wimbo ulio bora ni mfano wa kisa cha mapenzi kati ya Mungu na watu wake. Tazama kwa makini Andiko lifuatalo: “Mpenzi wangu, u mzuri pia wala ndani yako hamna ila.” (Wimbo ulio Bora 4:7).

Mungu anakupenda na kuona wema ulio ndani yako. Si hilo linastaajabisha? Bila shaka hicho ni kitu cha kushukuru! Mungu huona vile unavyokuja kuwa na vile utakavyokuwa; Hajali sana kuhusu makosa yako. Aliyajua yote alipokualika kuwa katika uhusiano wa ndani Naye.

Kile Mungu anataka ni upendo wako na hiari ya kukua ndani yake. Uwepo wako ni zawadi kwa ulimwengu. Wewe ni wa kipekee na wa aina ya kipekee. Usiwahi kusahau, hata kwa siku moja, vile ulivyo spesheli!


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kuwa Neno lako linanionyesha tu vile unavyonipenda. Haijalishi vile huenda wengine wakasema au vile mimi mwenyewe ninavyohisi, ninachagua kuamini kwamba ninapendwa sana na niliumbwa kiajabu na Baba yangu wa mbinguni.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon