Pita Mitihani Yako

Lakini, Ee Bwana wa majeshi, uhukumuye haki, ujaribuye nia na moyo… kwa maana nimekufunulia wewe neno langu. —YEREMIA 11:20

Maisha yetu yote yamejawa na changamoto zinazopima maamuzi na ukakamavu wetu na ubora wa tabia zetu—mitihani inayoweza kukutia nguvu na kukuleta katika uhusiano wa kina na Mungu. Inatusaidia kujijua kikweli, na husaidia katika kujua maeneo dhaifu katika tabia zetu.

Kitu hujaribiwa vipi? Shinikizo huwekwa ili kuona kama kitafanya kazi kwa njia nzuri. Mungu huruhusu mitihani kuja katika maisha yetu ili kuonyesha nguvu na udhaifu wetu, na lengo letu wakati wote linafaa kuwa kupita mitihani yetu, sio kuiepuka. Mitihani huja kabla ya kuinuliwa! Ukitaka kuinuliwa, itabidi ufanye na kupita mitihani yako kutoka kwa Mungu.

Mtume Yakobo alieleza kwamba mitihani hutoa vitu vilivyo ndani yetu (Yakobo 1:2-4), na bila shaka nimetambua kwamba ni kweli kabisa. Huwa inatuonyesha maeneo ambayo tumekua katika Mungu, na maeneo ambayo bado tunahitaji usaidizi. Hiki ni kitu kizuri, kwa sababu hatuwezi kuboreka katika eneo lolote iwapo hatujui mahali udhaifu wetu upo.


Tabia kwa kweli hudhihirika shinikizo linapotumiwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon