Upendo Huonyesha Heshima

Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. —WAFILIPI 4:5

Upendo ni tendo la ukarimu, na kujitolea. Mtu mchoyo hutarajia kila mtu kuwa vile alivyo na kupenda chochote anachopenda, lakini upendo huheshimu tofauti zilizo ndani ya watu wengine.

Kuheshimu haki binafsi za mtu ni muhimu sana. Iwapo Mungu angetaka sisi wote tufanane, asingempa kila mmoja wote alama tofauti za vidole. Ninafikiri huo ukweli mmoja peke yake unathibitisha kwamba tumeumbwa kwa usawa, lakini na utofauti. Sisi wote tuna alama za vidole, lakini zote ni tofauti!

Sisi wote tuna uwezo tofauti, vitu tofauti tunavyopenda na tusivyopenda, misukumo tofauti, na orodha inaendelea na kuendelea. Tunaonekana tofauti, tunakuja kwa saizi zote na maumbo, na kila moja wetu ni wa pekee.

Upendo huweka huru kwa heshima wengine ili wawe kile walichoumbwa kuwa. Uhuru ndicho mojawapo ya vipawa vikuu tunavyoweza kupeana. Ndio ambao Yesu alikuja kutupatia, na ndio upendo unaoturuhusu kuwapa wengine.

Upendo wa Mungu juu yetu hauna masharti, na tunafaa kujifunza kupenda wengine vivyo hivyo. Kuwa mkarimu na mwenye rehema na utumainie mema.


Upendo usio na masharti hupenda watu wabinafsi bila choyo, huwa mkarimu kwa watu wachoyo, na kuwabariki bila kukoma watu wasio na shukrani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon