Uweza wa “MIMI NIKO AMBAYE NIKO”

Uweza wa “MIMI NIKO AMBAYE NIKO”

Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO ambaye NIKO; akasema ndivyo utakawavyowaambia wana wa Isreali; MIMI NIKO amenituma kwenu! —KUTOKA 3:14

Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, MIMI NIKO. —YOHANA 8:58

Mungu alipomwambia Musa—na Yesu alipowaambia wanafunzi wake—“MIMI NIKO,” alikuwa anasema kitu cha ajabu sana. Ni kitu ambacho kinaweza kubadilisha vile tunavyoishi maisha yetu ya kila siku tukikiamini kwa kweli.

Mungu ni mkubwa sana, hakuna neno linalotosha kueleza alivyo. Tunaweza vipi kueleza kwa jina moja mtu ambaye haelezeki? Mungu sio kitu kimoja tu—ni kila kitu. Ndiyo kwa sababu Mungu alikuwa akimwambia Musa, MIMI NIKO ninaweza kushughulikia kila kitu utakachokabiliana nacho. Chochote unachohitaji, MIMI ni hicho. Hakuna kitu nisichoweza kushughulikia. Nimefanya kila kitu, sio tu wakati huu bali nyakati zote. Unaweza kutulia, kwa sababu MIMI NIKO. Niko nawe na Ninaweza kufanya yanayohitaji kufanywa!

Hilo ni kweli kwako leo pia. Chochote unachohitaji, Mungu ni MIMI NIKO. Ndani yake utapata kutimiziwa mahitaji, furaha, amani, uponyaji, urejesho na nguvu. Hata kabla ujue unachohitaji, MIMI NIKO anajua, na yuko hapo wakati wote kutupatia kila kitu chema.


Hakuna cha kuogopa maishani ukijua kwamba unaweza kupata kwa urahisi wema, neema na nguvu za MIMI NIKO zisizo na kikomo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon