Zaidi ya Vitu

Zaidi ya Vitu

Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokitaka kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. WAFILIPI 4:19

Mara nyingi huwa tunaona mahitaji kuwa haja za kimsingi katika maisha yetu—chakula, makao, mavazi na pesa za kununua vitu hivi. Hivi huwakilisha mahitaji yetu ya kimwili, lakini Mungu alituumba kuhitaji zaidi ya hivi. Mahitaji yetu yanatofautiana.

Hatuhitaji tu pesa, lishe bora au makao na mavazi ya kuvaa. Tunahitaji pia hekima, nguvu, afya, marafiki, na wapendwa; na tunahitaji vipaji na vipawa vya kutusaidia kufanya yale tunahitaji kufanya maishani. Tunahitaji vitu vingi, na, shukuru kwamba, Mungu anahiari kutimiza mahitaji yetu yote tunapomtii na kumwamini.

Lazima tuamini kwamba anataka kutupatia halafu uanzishe nia ya kutoa shukrani kwa kile alichofanya na anachokifanya.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru leo kwa kipaji cha upaji wako. Hutimizi tu baadhi ya mahitaji yangu, unatimiza mahitaji yangu yote. Asante kwa upaji wako mkamilifu kabisa ambao hunipitisha katika kila siku ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon