
TUMAINI kwa nyakati ngumu
Unapita katika kipindi kigumu? Iwe unashughulikia msiba au tatizo ambalo haukulitarajia, ugonjwa wa kutisha unaohitaji matibabu, au hata unajiuliza mlo wako unaofuata utatoka wapi, Mungu hataki ukabiliane na vita ukiwa peke yako. Badala yake, jambo kuu moja tunaloweza kufanya ni kumwamini Yeye, tukijua kuwa yuko pamoja nasi na tunaweza tukabaki tukiwa tumejaa matumaini.
Katika kitabu hiki, Joyce anafundisha:
- Namna ya kupokea faraja ya Mungu katika nyakati ngumu
- Kwa nini mabadiliko ya mtazamo yanaweza yakaibadilisha kabisa siku yako
- Namna ya kuanza upya na kusahau mambo ya zamani
- Funguo za Kibiblia za kupambana na unyogovu na kuvunjika moyo
Chochote ulichopitia, kitabu hiki kitakusaidia kuongeza matarajio yako na usikate tamaa kwa Mungu kamwe. Kwa sababu, zaidi ya yote, Yeye ndiye “Mungu wa tumaini” (Warumi 15:13), na Yeye ndiye anaweza kuichukua hali yako na kuibadilisha kuwa kitu kizuri zaidi.

Tumaini Dhabiti
Mungu hufurahia kutushangaza na atafanya hivyo kila mara iwapo tutaachilia vitu katika mikono yake na usalama wake. Anataka tushirikiane katika maisha yetu, na tukimruhusu kufanya hivyo, nafsi zetu zinaweza kuwa na utulivu.
MAGEUZI YA UPENDO
Ninapokaa na kunywa kahawa yangu asubuhi, nikiangalia kupitia...
Nisaidie-Ninaogopa! (629KB)
Ujumbe huo, “Usiogope, kwa maana Mimi Mungu, niko pamoja nawe,” umeashiriwa mara nyingi sana katika Biblia.