MAGEUZI YA UPENDO

Ninapokaa na kunywa kahawa yangu asubuhi, nikiangalia kupitia dirisha la nyumba yangu mandhari nzuri ya makazi yangu, watu milioni 963 wana njaa. Zaidi ya watu bilioni moja wana mapato ya chini ya dola moja kwa siku. Watoto elfu thelathini watakufahivi leo kwa sababu ya umaskini. Wanafariki katika baadhi ya vijiji maskini zaidi duniani wakiwa mbali kabisa kufikiriwa na ulimwengu. Hii inamaanisha kwamba watoto 210,000 hufariki kila wiki, milioni 11 kila mwaka na wengi wao wako chini ya umri wa miaka mitano.

Kati ya watoto bilioni 2.2 walioko duniani, milioni 640 hawana makazi, milioni 400 hawapati maji safi ya kunywa na milioni 270 hawapati huduma zozote za matibabu hata iweje.

Kupakua
MAGEUZI YA UPENDO
Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon