Tumaini Dhabiti

Tumaini hutuwezesha kuishi bila uzani, mizigo au tahadhari kwa sababu huwa tuna hakika kuwa kunaye atakayeshughulikia mambo kwa niaba yetu. Badala ya kuhisi kwamba tunabeba mzigo mzito kila wakati, tunaweza kufurahia wepesi wa ajabu katika nafsi zetu. Ili kuweka tumaini letu ndani ya Mungu na kumwachia mizigo yetu, tunahitaji kufanya uamuzi. Daudi alizungumza juu ya kuweka tumaini lake kwa Mungu kila wakati. Neno “weka” ni neno la kitendo ambalo tunalipata katika Neno la Mungu kila wakati anapotupatia maagizo kuhusu jambo ambalo angependa tufanye- mambo kama jivikeni upendo, vaeni utu mpya, fungeni miguu kwa injili ya amani na pia kumtumaini Mungu (Wakolosai 3:14, Waefeso 4:24, Waefeso 6:15, Mithali 3:5)

Kupakua
Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon