TUMAINI kwa nyakati ngumu

Unapita katika kipindi kigumu? Iwe unashughulikia msiba au tatizo ambalo haukulitarajia, ugonjwa wa kutisha unaohitaji matibabu, au hata unajiuliza mlo wako unaofuata utatoka wapi, Mungu hataki ukabiliane na vita ukiwa peke yako. Badala yake, jambo kuu moja tunaloweza kufanya ni kumwamini Yeye, tukijua kuwa yuko pamoja nasi na tunaweza tukabaki tukiwa tumejaa matumaini.

Katika kitabu hiki, Joyce anafundisha:

  • Namna ya kupokea faraja ya Mungu katika nyakati ngumu
  • Kwa nini mabadiliko ya mtazamo yanaweza yakaibadilisha kabisa siku yako
  • Namna ya kuanza upya na kusahau mambo ya zamani
  • Funguo za Kibiblia za kupambana na unyogovu na kuvunjika moyo

Chochote ulichopitia, kitabu hiki kitakusaidia kuongeza matarajio yako na usikate tamaa kwa Mungu kamwe. Kwa sababu, zaidi ya yote, Yeye ndiye “Mungu wa tumaini” (Warumi 15:13), na Yeye ndiye anaweza kuichukua hali yako na kuibadilisha kuwa kitu kizuri zaidi.

Kupakua
TUMAINI kwa nyakati ngumu
Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon