Ombi kwa ajili ya Kuokoka

Ombi kwa ajili ya Kuokoka

Mungu anakupenda, na anataka kuwa na uhusiano wa kibinafsi nawe. Ikiwa hujampokea Kristo kama mwokozi wako, unaweza kufanya hivyo  hivi sasa. Fungua moyo wako kwake na uombe ombi hili.

“Baba, najua kwamba nimetenda dhambi mbele zako. Naomba unisamehe. Nioshe niwe safi. Naahidi kumtumaini Yesu Mwanao. Naamini kwamba alinifia- Alijichukulia dhambi yangu alipokufa  msalabani. Naamini kwamba alifufuliwa kutoka kwa mauti. Nayasalimisha maisha yangu kwa Yesu  hivi sasa.

Asante Baba, kwa kipawa chako cha msamaha wa dhambi na uzima wa milele. Tafadhali niwezeshe kukuishia, katika jina la Yesu, Amina”

Kwa vile umeomba kutoka moyoni mwako, Mungu amekupokea,amekuosha na kukuweka huru kutokana na utumwa wa mauti ya kiroho. Chukua muda usome na kuelewa maandiko haya na umuulize Mungu akunenee unapotembea naye katika safari hii ya maisha mapya.

Yohana 3:16 1 Wakorintho 15:3-4 Waefeso 1:4 Waefeso 2:8-9
1Yohana 1:9 1 Yohana 4:14-15 1 Yohana 5:1 1 Yohana 5:12-13

Muombe Mungu akuwezeshe kupata kanisa ambalo linaamini mafunzo ya bibilia ili uweze kuhimizwa kukua katika uhusiano wako na Kristo. Mungu yuko nawe kila mara. Atakuongoza siku baada ya siku na kukufunza jinsi ya kuishi maisha ya utele aliyonayo kwa ajili yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon