Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba wala mauti wala uzima wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. Warumi 8:38–39
Ili kuelewa kikamilifu pande zote tofauti za upendo, lazima tuelewe kuna aina mbili za upendo: aina ya upendo wa Mungu na upendo wa binadamu.
- Upendo wa binadamu hupungua, hukata tamaa; lakini wa Mungu haupungui.
- Upendo wa binadamu hukoma, huisha, lakini wa Mungu haukomi ni wa milele.
- Upendo wa binadamu ni wa kutegemea tabia na hali nzuri; upendo wa Mungu hautegemei matendo yetu
- Watu huweka masharti kwenye upendo wao, lakini upendo wa Mungu hauna masharti.
Huu upendo usiopungua, usio na kikomo na usio na masharti ndio upendo ambao Mungu anao kwa ajili yako kila siku. Kuwa mwenye shukrani kwa upendo wake; sherehekea upendo wake; na uwe salama maishani kwa sababu unajua una upendo usio na masharti na ukubalifu wa Baba yako wa mbinguni.
Sala ya Shukrani
Baba, nisaidie kusherehekea upendo wako mtimilifu usio na masharti leo. Ninakushukuru kwamba upendo wako ni wa juu kuliko upendo wa binadamu, na ninashukuru kuwa unaninyoshea upendo huo kila siku.