
Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele. Zaburi 55:22
Je, unajua kwamba Mungu anataka kufanya biashara na wewe? Anataka umpe masuala yako yote, matatizo na kushindwa kwako. Badala yake, Yeye atakupa amani na furaha yake.
Kwa kweli Mungu anataka kututunza, lakini ili kumruhusu, tunapaswa kuacha kujaribu kujitunza wenyewe na kuhangaika juu ya kila kitu kidogo ambacho hatuwezi kudhibiti. Watu wengi wangependa Mungu awajali, lakini wanasisitiza juu ya wasiwasi au kujaribu kupataa majibu wao wenyewe, badala ya kusubiri mwongozo wa Mungu.
Mungu atatupa amani, lakini tunapaswa kwanza kumpa wasiwasi wetu. Ni biashara kubwa! Tunampa Mungu wasiwasi wetu, na Yeye anatupa amani Yake. Tunampa wasiwasi wetu wote na hoja zetu, naye anatupa ulinzi wake, utulivu na furaha. Hiyo ni baraka ya ajabu na fursa ya kuzingatiwa naye.
OMBI LA KUANZA SIKU
Bwana, umenipa biashara ya kushangaza. Wewe una uwezo zaidi kuniliko, kwa hiyo ninakupa wasiwasi yangu yote na kupokea amani yote na furaha Unayonipa!