Furaha Zaidi

Furaha Zaidi

Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa. —MITHALI 17:22

Ufahamu wangu wa furaha ni kwamba, hufunika hisia tofauti, kuanzia kwa utulivu unaopendeza hadi kwenye burudani. Nyakati za burudani hufurahisha, na sisi wote tunahitaji hizo nyakati za kucheka hadi mbavu zetu zivunjike. Bila shaka hatuwezi kuishi maisha yetu ya kila siku hivyo, lakini tunahitaji nyakati hizo, kwa kuwa, “Kwa nini basi Mungu akatupa uwezo wa kucheka?”

Kama Wakristo tunaweza kukua katika uwezo wetu wa kufurahia maisha na kuweza kusema, “Ninaishi maisha yangu katika hali ya utulivu wa kupendeza.” Ninafikiri utulivu wa kupendeza ni mchanganyiko wa amani na furaha.

Baadhi ya maneno ya Kigiriki yanayohusiana na neno furaha katika Biblia yanamaanisha kupendeza, shangwe, nderemo, msisimko, raha, furaha kuu. Nimesikia likifafanuliwa pia kama raha au furaha kuu au chanzo cha raha au kuridhika, kujazwa na furaha au kufurahia.

Haijalishi ufananuzi utakaopendezwa nao, ukweli wa kuhuzunisha ni kwamba waaminio wengi sana hawafahamu furaha ya Bwana. Usiache siku nyingine ipite bila kufurahia kitovu cha ufalme wa Mungu—haki, amani, na furaha ndani ya Roho Mtakatifu (Warumi 14:17).


Hakuna jambo la kuhuzunisha kama kuwa hai na kukosa kufurahia maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon