Karama ya Unabii

… na mwingine unabii… (WAKORINTHO 12:10)

Karama ya kweli ya unabii iko katika kutumika, mtu anaposikia na kusema ujumbe ulio wazi kutoka kwa Mungu kwa mtu mwingine, kikundi, au hali. Wakati mwingine unabii huwa wa kijumla na wakati mwingine ukawa maalum. Unaweza kuja kupitia kwa mahubiri au ujumbe uioandaliwa, au huenda ukaja kwa ufunuo wa kiungu.

Ingawa karama ya unabii ni muhimu sana, kwa bahati mbaya, umetumiwa vibaya na kusababisha rabsha nyingi. Bila shaka kuna manabii wa kweli leo, lakini pia wapo manabii wa uongo. Halafu kuna wale wasiokusudia kudhuru wanapojaribu kusema neno kutoka kwa Mungu, lakini wanfanya hivyo kutoka kwa ufahamu wao, hiari au hisia badala ya, kwa Roho wa Mungu.

Makusudio na malengo ya unabii wa kweli ni “kujenga na kuinua kiroho na kuhimiza na kufariji” watu (1 Wakorintho 14:3). Karama zote za Roho Mtakatifu ni za wema na faida ya wote. Isitoshe, neno la kweli litaambatana na amani na “kutulia” moyoni mwako na rohoni kwamba limetoka kwa Mungu; litathibitisha pia kitu ambacho tayari kiko moyoni mwako, hata kama ni kwa mbali. Kigezo hiki kinaweza kusaidia kutambua iwapo unabii ni wa kweli au la. Bila shaka, kipimo cha kweli cha unabii ni iwapo utakuja kutimia au la. Kumbuka hili: Unabii wa kweli hutimia. Sio wale walio na karama ya unabii peke yao wanaosikia kutoka kwa Mungu. Una uwezo na haki ya kujisikilia sauti yake, kwa hivyo zijaribu roho zinazotumikishwa kwa unabii unaopokea na uzijaribu ili uhakikishe kwamba zinatoa ushahidi katika moyo wako (soma Yohana 4:1).

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Watu wakikupa ushauri na kukuambia kuwa umetoka kwa Mungu, hakikisha unakubaliana na Neno la Mungu na kuthibitishwa katika moyo wako mwenyewe.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon