Kila Kipawa Kizuri

Kila Kipawa Kizuri

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.. — YOHANA 1:16

Mimi na wewe tunaweza kuishi katika ushindi leo kwa maana Roho Mtakatifu anatuwezesha katika maisha na kutufundisha kuomba. Anatusaidia kuomba Mungu tunachohitaji badala ya kujaribu sisi wenyewe kufanya vitu vifanyike.

Roho Mtakatifu ndiye anayeleta kipawa chema katika maisha yako, kila unachohitaji. Majukumu yake mengi kama Mfariji, Mshauri, Msaidizi, Muombezi, Mtetezi, Mtia Nguvu na Aliye hapo wakati wote yanaweza kufupishwa kwa kusema kwamba kusudi lake ni kutukaribia kabisa iwezekanavyo na kufanya maisha yetu yafanikiwe kwa utukufu wa Mungu.

Mungu anataka kujua kila kitu kidogo kuhusu maisha yako. Anataka kukusaidia kila kitu katika maisha yako. Husimama kando yetu wakati wote akingoja nafasi ya kwanza itakayotokea ili aingie na kutupatia usaidizi na nguvu tunazohitaji. Omba usaidizi kila mara unapouhitaji. Hatuna kwa sababu hatujaomba (Yakobo 4:2), kwa hivyo omba, na uombe na uombe. Endelea kuomba ili upokee na furaha yako iwe timilifu (Yohana 16:24).


Kazi ya Mungu ni kutupatia neema na Roho wake; kazi yetu ni kuomba usaidizi wake na kujitwaa kwake kama vyombo ili kupitia kwavyo afanye kazi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon