Kujazwa na Mungu

Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo…na kuujua upendo wake Kristo , upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu (WAEFESO 3:17, 19)

Kujazwa na uwepo na uwezo wa Mungu ni jambo la ajabu na, kulingana na andiko la leo, ni mapenzi ya Mungu kwetu sisi. Kujazwa na Mungu ni bora kuliko kujazwa na ubinafsi. Ubinafsi ni njia ya kuishi kwa dhiki, lakini Mungu ametoa njia ya sisi kumwishia na kuishia wengine, kupitia kwa Yesu Kristo.

Biblia inafundisha kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya wote, “ili waliyo hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao” (2 Wakorintho 5:15). Yesu ametutengenezea sisi njia ya kuwa na maisha ya ajabu, yaliyojaa amani na furaha. Ametufanyia njia ya kupenda wengine badala ya kuishi kwa sababu ya raha na makusudio yetu.

Ili kujazwa na uwepo wa Mungu, unahitajika kumtafuta, kusoma Neno lake, na kuwa na tabia zinazompa nafasi katika maisha yetu. Kuanza siku yako na andiko na ushirika na Mungu ni njia ya kuanzisha siku yako vizuri. Siku hii ni zawadi ya Mungu kwako, kwa hivyo usiiharibu. Anangoja kukujaza kwa uwepo wake, kwa hivyo omba na upokee ili furaha yako ikamilike.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Jazwa na Mungu na umruhusu kugusa wengine kupitia kwako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon