Kujifunza Kuvumilia Kukosolewa

Kujifunza Kuvumilia Kukosolewa

Kwa tumaini, mkifurahi katika dhiki, mkisubiri katika kusali, mkidumu… WARUMI 12:12

Haijalishi tunachofanya maishani, kuna wakati maishani ambapo sisi wote tutakabiliana na kiwango fulani cha ukosoaji. Lakini inawezekana kujifunza vile unavyoweza kuvumilia kukosolewa bila kuathirika kimaisha.

Tunaweza kushukuru kwa mfano ambao Mtume Paulo alitupatia. Paulo alikosolewa kila mara, lakini akasema hakuwa na wasiwasi kuhusu hukumu ya wengine. Alijua alikuwa mikononi mwa Mungu na kwamba mwishowe atasimama mbele ya Mungu na kumpa habari zake na maisha yake. Hatasimama mbele ya mwanadamu yeyote kuhukumiwa (tazama 1 Wakorintho 4:3–4).

Huenda usifanye kila kitu kwa njia sahihi kila wakati, lakini Mungu huona moyo wako. Iwapo unajaribu kuishi kwa ajili ya Mungu na kutafuta njia za kuwapenda wengine, Mungu anafurahishwa nawe (tazama Mathayo 22:37–40). Usijali kuhusu ukosoaji wa wengine; Mungu anakupenda. Unachohitaji ni upendo na kibali chake.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba sihitaji kusikiliza ukosoaji wa wengine. Unaona moyo wangu na unajua nia zangu. Ninakushukuru kuwa kibali chako ni kikuu kuliko kibali cha mtu yeyote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon