Umngoje Bwana, uwe hodari, upige moyo konde, naam umngoje Bwana. —Zaburi 27:14
Tukimngoja Mungu, hatuwi wavivu au kukosa kujishughulisha, lakini kwa kweli tunajishughulisha kabisa kiroho. Huenda tusiwe “tunafanya” kitu, lakini tunamwamini Mungu kufanya yanayohitajika kufanywa. Kwa maneno mengine, tunasema, “Bwana, sitajaribu kufanya haya kwa nguvu zangu. Nitakungoja uniokoe. Na nitaendelea kufurahia maisha yangu huku nikikungoja.”
Shetani anataka tusikitike kutokana na kujaribu kutatua matatizo yetu wenyewe. Anachukia furaha yetu. Anataka kuona kitu kingine lakini si furaha, kwa sababu furaha ya Bwana ni nguvu zetu (Nehemia 8:10). Wasiwasi huiba furaha yetu, lakini furaha hututia nguvu.
Huwa tunajaribiwa kufikiri hatufanyi yanayotupasa kufanya tusipokuwa na wasiwasi au kutafuta jibu la matatizo yetu, lakini hili litazuia wokovu wetu badala ya kuusaidia. Si kutowajibika kufurahia maisha huku tukimngoja Mungu na kumtarajia kufanya kile tusichojua kukifanya!
Usihofu kwa kuwa vita si vyako, ni vya Bwana.