Kutazama Mbele

Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, tazama nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. —UFUNUO WA YOHANA 21:5

Watu wengi huishi maisha ya dhiki kwa sababu wana vita vya ndani kwa ndani na kuhisi uzito wa mizigo ya makosa yao ya zamani. Iwapo huna furaha na umekata tamaa kwa sababu ya vitu ambavyo vilifanyika katika maisha yako zamani, ninakuhimiza kubadilisha vile unavyofikiria na kuwa mwelekeo mpya. Amua kuwa kile Mungu anataka uwe, kuwa na kile Mungu anataka uwe nacho, na kupokea kile Yesu alikufa ili akupe.

Maisha yako mapya ndani ya Kristo yanamaanisha kwamba umesamehewa dhambi kabisa dhambi zako zote. Mungu amekupangusa na kukuanzishia upya maisha yako na kufanya makazi katika moyo wako. Unaweza kusahau yaliyopita na uanze kufurahia mstakabali wako.

Unapohisi kukata tamaa, sema, “Sitaishi katika utumwa tena. Siwezi kufanya lolote kuhusu yale nilifanya zamani, lakini naweza kufanya kitu kuhusu mustakabali wangu. Nitaanza kufurahia maisha yangu na kuwa na kile Yesu alikufa ili niwe nacho. Nitasahau yaliyopita na kuendelea kumtafuta Mungu kuanzia leo na kuendelea!”


Jana ni historia. Kesho ni siri. Leo ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon