Kuwa Na Fikra Chanya

Kuwa na Fikra Chanya

. . . Maana ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. —1 Wakorintho 2:16

Tangu nianze kuiweka nia yangu katika ruwaza chanya, siwezi kuvumilia hisia ya kuwa hasi. Nimeona mabadiliko mengi mazuri katika maisha yangu tangu niwekwe huru kutokana na nia hasi kiasi kwamba sasa ninapinga kitu chochote hasi.

Hili hapa ninalopendekeza, iwapo umeng’ang’ana kuishi kwa njia chanya: Mwambie Roho Mtakatifu akuhukumu kila wakati unapoanza kuwa hasi. Hiyo ni sehemu mojawapo ya kazi yake. Yohana 16:7-8 inatufundisha kwamba Roho Mtakatifu atatuhukumu kuhusu dhambi na kutuhakikishia haki. Hukumu itakapokuja, mwambie Mungu akusaidie. Usifikirie kwamba unaweza kukabiliana na hili mwenyewe. Mwegemee

Kuwa chanya haimaanishi kwamba hatukabiliani na ukweli. Biblia inasema kufanya yote ambayo hali ya hatari inadai halafu kusimama imara mahali pako (Waefeso 6:13). Mahali petu pako “ndani ya Yesu,” na ndani yake tunaweza kuwa na tumaini tele na kuwa na fikra chanya kwa sababu hakuna kilicho kigumu sana kwake. Yesu alikuwa na fikra chanya kila wakati na mwingi wa imani. Tuna nia yake ndani yetu, na kwa usaidizi wake, tunaweza kufanya vitu vivyo hivyo.


Waza kama Mungu, ili uweze kuwa mtu ambaye anataka uwe na kuwa na yote anayotaka uwe nayo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon