Mahusiano Yaliyo Huru Kutokana na Migogoro

Mahusiano Yaliyo Huru Kutokana na Migogoro

Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao. 2 TIMOTHEO 2:14

Amani ni kiambato muhimu kwa maisha ya furaha, lakini haitoshi tu kutamani amani. Lazima tufuatilie amani katika uhusiano wetu na Mungu na uhusiano wetu na watu wengine. Paulo alifahamu vile amani inavyoweza kuwa telezi isipokuwa tukiitafuta kwa bidii, kwa sababu katika barua zake nyingi, anawasihi waaminio kuishi katika umoja.

Ili kuishi kwa kupatana, tunafaa kushukuru kwa ajili ya kila mmoja wetu, kutenga nafasi kwa ajili ya wengine, na kupuuza makosa na upungufu wa kila mmoja. Tunafaa kuwa wanyenyekevu, wenye upendo, huruma, na uungwana. Wakati wote uwe unahiari kusamehe haraka na kila mara, na usiwe wa kuudhiwa haraka.

Umoja, kupatana na kusikizana yote ni amani, na tunaweza kuwa nayo yote tukiyatafute kwa moyo wetu wote na tuhiari kuwa wapatanifu tunapoishi maisha haya.


Sala ya Shukrani

Baba, ninapokuwa katika hali ambapo ninajaribiwa kulalamika au kubishana, nisaidie kuwa mpatanishi badala yake. Ninakushukuru kwa tunda la kiasi katika maisha yangu. Na ninakushukuru kwa kuwa ninaweza kuishi kwa upatanifu na wale walio karibu nami.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon