Kwa maana macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. —2 MAMBO YA NYAKATI 16:9
Ina maana gani kuwa na moyo uliokamilika? Ina maana kwamba una matamanio ya ndani ya moyo ya kutenda mema na kumpendeza Mungu. Mtu aliye na moyo uliokamilika humpenda Mungu kwa kweli, ingawa huenda yeye mwenyewe asiwe mkamilifu au bila mawaa katika njia zake zote. Huenda bado ana udhaifu. Huenda akafanya makosa au kuwa na hasira. Lakini akifanya hivyo, huwa mwepesi wa kutubu na kupokea msamaha wa Mungu. Iwapo amemkosea mtu, atajinyenyekeza na kuomba msamaha. Kwa sababu moyo wake umemwelekea Mungu kwenye haki, ni rahisi kwa Roho Mtakatifu kumfundisha.
Mungu anapotafuta wale atafanya kazi kupitia kwao, hatafuti mtu wa matendo yaliyokamilika. Iwapo mmoja wetu angekuwa na tabia iliyokamilika, tusingemhitaji Yesu. Hata hivyo tunaweza kumpenda Mungu, na tukifanya hivyo, anajionyesha mwenye nguvu kwa ajili yetu.
Mungu huwatia nguvu wale wenye nia nzuri ya roho kwake.