Mungu Anakujali

Mungu Anakujali

Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. —1 Petro 5:7

Wasiwasi, dukuduku na fadhaa hayana matokeo chanya kwa maisha yetu. Hayaleti suluhisho kwa matatizo yetu. Hayatusaidii kupata afya nzuri, na huzuia ukuaji wetu katika Neno la Mungu.

Mojawapo ya njia ambazo Shetani huiba Neno la Mungu kutoka kwa mioyo yetu ni kupitia kwa fadhaa. Biblia inasema tumtwike Mungu fadhaa zetu, ambalo hufanywa kwa maombi. Hatuwezi kushughulikia shida zetu, hatukujengwa na uwezo huo. Tumeumbwa na Mungu kumtegemea, kumletea changamoto zetu, na kumruhusu kutusaidia.
Si busara kujitwika fadhaa za maisha wenyewe. Kuweka fadhaa zetu ni dalili ya kiburi. Inaonyesha kwamba tunaweza kutatua shida zetu wenyewe na kwamba hatumhitaji Mungu.

Tunaonyesha unyenyekevu wetu kwa kumwegemea Mungu. Wasiwasi, dukuduku, na fadhaa si dalili ya kumwegemea Mungu, lakini zinaeleza kwa kuwepo kwake kuwa tunajaribu kujikimu.
Omba kuhusu kila kitu na usiwe na wasiwasi kuhusu chochote. Utafurahia maisha hata zaidi.


Wasiwasi ni kama kubembea kitini: inakushughulisha bila kukufikisha popote!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon