Mungu Anataka Kukubariki

Mungu Anataka Kukubariki

. . . Bali wamtafutao Bwana hawatahitaji kitu chochote kilicho chema. ZABURI 34:10

Baadhi ya watu wamefundishwa kwamba kuteseka na kupungukiwa ni maadili katika maisha ya Kikristo. Kuweza kudumisha nia nzuri katika nyakati za kuteseka ni maadili ambayo ni muhimu sana, lakini kuendelea kuteseka sio mapenzi ya Mungu kwa yeyote. Hatufai kumwona Mungu kama Mungu mchoyo ambaye atatunyima kitu tunachokihitaji. Fikira hii mistari:

  • “Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. (Zaburi 23:1).
  • “Naam, waseme daima, atukuzwe Bwana, apendezwaye na amani ya mtumishi wake” (Zaburi 35:27).
  • “Atawabariki wamchao Bwana, wadogo kwa wakubwa” (Zaburi 115:13).

Mungu ni Baba mwema ambaye anapenda kuwabariki wanawe. Mungu anataka kukubariki na kukuona ukifurahia maisha yako! Unaweza kuwa tu mwenye shukrani, uzipokee, na uamini mazuri ya Mungu kwa bidii leo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwa kuwa wewe ni mwema, unanipenda na unataka kunibariki. Asante kwa kuwa sihitaji kuogopa kwa sababu utanilisha, kuniongoza na kunilinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon