Nguvu na Udhaifu

Kusimama Imara

Walilia, naye Bwana akasikia, akawaponya na taabu zao zote. ZABURI 34:17

Sisi wote tuna baadhi ya nguvu na udhaifu. Hili ni kweli hata kuhusu watu tunaosoma katika Biblia. Paulo alipigana na udhaifu wake (tazama 2 Wakorintho 12:9), lakini alijifunza kushukuru kwa ajili ya hiyo kwa kuwa kupitia kwa udhaifu huo, alitambua nguvu na neema ya Kristo hutosha.

Tukitaka kufurahia kikamilifu uzima ambao Mungu ametupatia, lazima tutambue neema ya Mungu inatosha kwa ajili ya udhaifu wetu pia—na kushukuru kwamba inatosha! Kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu, tunaweza kujua sisi ni akina nani katika Kristo na tusihukumike kwa sababu ya udhaifu wetu. Mwegemee Bwana, na uamini kwamba neema na nguvu zake ni kuu kuliko udhaifu wetu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwamba katika udhaifu wangu, unadhihirisha nguvu zako. Nguvu na neema zako zinanitosha vile zilivyomtosha Paulo. Asante kwa nguvu zako za kila siku katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon