Nia Nzuri Ina Athari

Ee Mungu uyasikie maombi yangu, uyasikilize maneno ya kinywa change (ZABURI 54:2)

Sisi wote tunataka maombi yetu yawe na athari na tunataka tuweze kuzungumza na Mungu kwa njia ambazo huleta moyo na mipango yake katika maisha yetu na maisha ya watu wengine kwa mafanikio. Biblia inasema, “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii” (YAKOBO 5:16). Tukitaka kuomba maombi yenye athari yanayonufaisha, basi tunahitaji kujua kinachoweza kusababisha yasiwe yenye athari. Maombi yetu yote huwa hayafanikiwi. Kwa mfano, wakati mwingine huwa tunataka kitu sana kiasi kwamba tunakosa kuomba kulingana na mapenzi yake- na maombi hayo hayana athari. Wakati mwingine huwa tumekasirika sana au kuumizwa mioyo hadi tunaomba maombi yaliyo na misingi yake katika hisia zetu badala ya Neno la Mungu au moyo wake- na hayo maombi si yenye athari vilevile.

Kupitia kwa Neno lake, Mungu hutuambia la kufanya ili tuombe maombi yenye athari. Maombi yenye athari hayatokani na kufuata utaratibu au kuzingatia kanuni fulani. Maombi yenye athari yana misingi yake katika Neno la Mungu; ni rahisi, ya uaminifu, na yaliyojawa  imani; hayafungwi katika kanuni au miongozo, lakini huhitajika kububujika  kutoka katika moyo wenye nia safi.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Nia mbaya inaweza kubadilishwa kwa kufanya uamuzi wa kuibadilisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon