Amin, nawaambia atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. —MARKO 11:23
Watu hufikiri kwamba maisha ni tata, lakini mara nyingi ni sisi tunaofanya mambo kuwa tata zaidi kuliko vile yanahitaji kuwa. Kumwishia Mungu si jambo la utata hata.
Fikiria kuhusu mtazamo rahisi usio na utata ambao mtoto anao juu ya maisha. Watoto huwa na burudani na kufurahia maisha yao bila kujali lolote. Huwa wana furaha tele tele, wasiojali, na bila wasiwasi wowote. Na watoto huamini kile wanachoambiwa. Ni kawaida yao kuamini kabisa na kufurahia maisha yao kila siku.
Kadri tunavyokua ndani ya Mungu, ndivyo tunavyokuwa kama watoto. Bila shaka, Mungu anataka tuwe wakomavu katika tabia zetu, lakini anatamani pia tuwe na nia ya kumtumainia na kumtegemea ambayo ina ukawaida kama wa mtoto. Mungu ananena na moyo wako au unaposoma kitu katika Biblia, unaweza tu kusema, “ Ninamwamini Mungu na ninaamini ni ukweli!” Ni rahisi hivyo.
Mungu anaposema atanifanikisha, ninamtumainia Mungu na kuamini ni kweli! Mungu akisema ataniponya, ninamtumainia Mungu na kuamini ni kweli! Mungu anaposema atanisaidia kusamehe walionidhuru, ninamtumainia Mungu na kuamini ni kweli. Mungu anaposema yuko nami na siko peke yangu, nimtumainia Mungu na kuamini ni kweli!
Kitu rahisi unachoweza kufanya ni kuamua kumtumainia Mungu na kutii Neno lake katika kila eneo la maisha yako.