Tembea kwa ujasiri

Tembea kwa ujasiri

Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Mithali 28:1

Watu wengine huwa na ujasiri, wakati wengine wanapambana na kuishi kwa ujasiri kama mtoto mpendwa wa Mungu. Nilikuwa na tatizo hilo mpaka Mungu aliponionyeshea funguo muhimu ambazo zimenisaidia kuishi kwa ujasiri, na nataka kuwashirikisha.

  1. Acha kuishi kwa hofu. Hofu ni janga katika jamii yetu. Biblia inatufundisha katika Waebrania 10:38 kuishi kwa imani na si kurudi nyuma kwa hofu.
  2. Weka vikwazo nyuma yako. Wewe hujashindwa kwa sababu unajaribu mambo mapya na hayafanyi kazi. Unashindwa tu wakati unapoacha kujaribu. Usiogope kufanya makosa, na kama unafanya, geuka haraka na uendelee.
  3. Acha kujilinganisha. Ujasiri hautawezekana kwa muda mrefu unapojilinganisha na wengine. Ujasiri huja kwa kukubali wewe ni nani na kuwa bora zaidi.
  4. Kuwa na nia ya kuchukua hatua. Chunguza moyo wako na ujiulize kile unachoamini Mungu anataka ufanye-na kisha ukifanye.

Omba juu ya funguo hizi nne na umuombe Roho Mtakatifu kukusaidia kuzishika. Katika Kristo, na kwa neema Yake, unaweza kuwa na ujasiri na kujazwa kwa ujasiri.

OMBI LA KUANZA SIKU

Roho Mtakatifu, nataka ujasiri kuwa moja ya sifa zangu za kunitambulisha. Nisaidie kuishi kwa funguo hizi nne kwa nguvu zako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon