Ufasiri wa Ndimi

…na mwingine tafsiri za lugha… (1 WAKORINTHO 12:10)

Mtu akizungumza katika ndimi katika mkutano wa ibada, lazima ujumbe huo ufasiriwe, kulingana na 1 Wakorintho 14:27. Wakati mwingine mimi hupewa ufahamu au fasiri za ujumbe uliotolewa katika ndimi. Zinakuja kwangu kama maelezo au kujua katika moyo wangu kile ambacho Mungu anajaribu kuwasilisha kwa wale wanaosikiliza.

Kwa madhehebu mengi ya Kikristo, vitu hivi ni siri tu kwa sababu hawajawahi kufundishwa kuvihusu. Ninaamini kwamba tunaishi katika nyakati ngumu na kwamba tunahitaji usaidizi wote wa kimiujiza tunaoweza kupata kutoka kwa Mungu. Ni muhimu kutodanganywa, lakini ni muhimu pia kutoogopa sana kudanganywa kiasi cha kuishia kujifungia nia kwa karama za Mungu.

Paulo alihimiza waaminio kuomba katika ndimi na kuomba kwamba waweze kufasiri, na ninaamini tunafaa kufanya hivyo hivyo. Kuwa na karama ya kufasiri kunatuwezesha kuelewa vizuri zaidi tunachoomba tunapotumia lugha yetu ya kibinafsi ya maombi. Fasiri ni tofauti na tafsiri. Hatupokei fasiri ya neno baada ya jingine lakini huwa zaidi uhisivu wa kijumla wa kile Mungu anawaambia watu wake.

Mungu ni Roho na sisi ni viumbe wa kiroho ambao lazima tujifunze kuhisi katika roho zetu kile Mungu anatuambia. Ninakuhimiza kujisomea hivi vitu mwenyewe na kumwomba Mungu ufahamu kuhusu karama zake zote za ajabu. Kitu muhimu ni kufungua nia yako na kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu unapoomba na kutafuta Mungu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kuwa na ujasiri na umwambie Mungu akuongoze katika ufahamu wa siri na maajabu yake.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon