Vyombo vya Heshima vya Uweza

Vyombo vya Heshima vya Uweza

Bwana Mungu amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemea kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha , sikio langu lipate kusikia kama watu… —ISAYA 50:4

Maneno ni vyombo vya heshima vya nguvu. Mungu aliumba ulimwengu kwa maneno yake (Waebrania 11:3). Roho Mtakatifu hubadilisha maisha kwa maneno. Yesu alisema kwamba maneno yake ni roho na uzima (Yohana 6:63).

Nguvu za maneno zinaweza kutumiwa kuinua watu au kuwashusha—inategemea vile tunavyochagua kutumia nguvu hizo kila siku. Watu hutiwa moyo au kushindwa kwa maneno tunayozungumza. Matamanio ya Mungu kwetu sisi ni kuwaonyesha watu upendo wake kupitia kwa kuwahimiza, na maneno chanya yanayotoa uzima. Kunenea mtu neno linalofaa na kwa wakati mzuri kunaweza kugeuza maisha yao yote.

Hilohilo ni kweli kuhusu maisha yetu binafsi. Tunaponena Neno la Bwana juu ya hali yetu, vitu huanza kubadilika. Maneno yana nguvu hivyo.

Hii ndiyo kwa sababu kujua Neno la Mungu ni muhimu sana. Tunaweza kulisoma, kujifunza, kisha tulitamke kulingana na hali zetu. Kwa mfano, unapohisi kutamauka, usiseme, “usiseme sitawahi kutoka katika hali hii.” Badala yake sema, “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu” (Zaburi 42:5). Utashangaa vile maisha yako yatabadilika utakapobadilisha vile unavyozungumza.


Fanya uamuzi kwamba maneno yako yatahimiza, kuinua, na kujenga maisha yako na maisha wengine wanaokuzunguka.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon