Tazama, nitatenda Neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. ISAYA 43:19
Umeshawahi kukumbana na hali na ukasema, “Hakuna vile hii inaweza kuwa?” Huenda fikra kama hizi zimo akilini mwako:
• Hakuna vile ninavyoweza kukabiliana na mshinikizo ulio kazini
• Hakuna vile ninavyoweza kulipa bili zangu
• Hakuna njia ya kuokoa ndoa yangu
• Hakuna njia ninayoweza kurudi chuoni sasa hivi
Kwa usaidizi wa Mungu, huwa kuna njia kila wakati. Huu ni ukweli mzuri unafaa kutufanya tushukuru. Huenda isiwe rahisi; huenda hali isiwe inafaa; huenda isije haraka. Huenda utalazimika kwenda juu, chini, karibu na au kupitia kwa matatizo—lakini kama utaendelea kukazana, utapata njia. Yesu alisema katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi Njia na Kweli na Uzima.” Yeye ndiye Njia, na atakusaidia kupata njia hata mahali ambapo inaonekana kwamba haipo.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwamba “umefanya njia katika jangwa.” Nisaidie kukutazama wewe na sio kwa hali zangu. Asante kwamba unanifanyia njia leo.