Wasiwasi au Ibada?

Wasiwasi au Ibada?

Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu. ZABURI 29:2

Wasiwasi ni kinyume cha ibada, na tunafaa kuwa na furaha zaidi ikiwa tumejifunza kuwa waabudio badala ya kuwa watu wa wasiwasi. Wasiwasi humpa adui nafasi ya kututesa, lakini ibada (kumcha na kusujudu Mungu) hutuongoza katika uwepo wake, mahali ambapo tutapata amani, furaha na tumaini kila mara.

Mungu alituumba tumwabudu. Anataka tujenge uhusiano wa ndani wa kibinafsi naye na upendo mkuu kwake. Aina hii ya upendo hutiririka kutoka kwa moyo wenye shukrani, kumkubali Mungu alivyo na yale amefanya.

Usiharibu siku nyingine ya maisha yako ukiwa na wasiwasi. Tambua wajibu wako na wajibu usio wako. Usijaribu kuchukua wajibu wa Mungu. Tunapofanya tunachoweza kufanya, Mungu anaingilia kati na kufanya kile tusichoweza kufanya. Kwa hivyo jipe kwake Mungu pamoja na wasiwasi zako, mwabudu, na uanze kufurahia uzima tele tele ambao amekupa.


Sala ya shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba ninaweza kuchagua kukuabudu badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu shida zangu. Nisaidie kuona kwamba wewe ni mkuu kuliko kizingiti chochote ninachokabiliana nacho, na ninaweza kukuamini kuwa utafanya nisichoweza kufanya katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon